Friday, September 14, 2018

KUNAMBI SERVICES

HIFADHI ,MAGAZETI YALIYOTUMINA NA UZA HAPA

WINNIE HOUSE OF SHINE

EPUKA KUPATA BIDHAA FAKE BOTUER ORIGINAL ZINAPATIKANA KWA WINNIE HOUSE OF SHINE

PIGA SIMU SASA. 0716971067 AU 0767370810 















Saturday, July 28, 2018

Rais amefanya mabadiliko madogo katika nafasi mbalimbali

Rais amefanya mabadiliko madogo katika nafasi mbalimbali
DjMtj2IXcAUEmxX.jpg

Rais John Magufuli amemteua Jokate Mwegelo kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe mkoa wa Pwani

Rais pia amemteua Jerry Muro kuwa Mkuu wa Wilaya ya Arumeru mkoa wa Arusha.

Patrobas Katambi ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Dodoma.

Wakati huo huo, David Kafulila ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Songwe.

Moses Machali ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu mkoa wa Mtwara

Lengay Ole Sabaya ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai mkoa wa Kilimanjaro

Daniel Godfrey Chongolo ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mkoa wa Dar Es Salaam.

Rais Magufuli amemteua Ally Hapi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa , kabla ya uteuzi huo Hapi alikuwa mkuu wa wilaya ya Kinondoni.

Dr Jim Yonaz ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mawasiliano

https://sagacious8.blogspot.com/

Wednesday, July 25, 2018

Juk square ft mussa baro

Muendelezo wa simulizi yetu ya ndoto sehemu ya 2 & 3

NDOTO SEHEMU YA PILI. 
Mtunzi:Francis Dickson
Mobile: 0757172326.
Publisher: Sagacious Blog


Nitakuwa nae.Tukafika sumbawanga ulikuwa usiku wa saa mbili,nikiwa na rafiki yangu namba ngeni ikapigwa katika simu yangu.. 
"Haloo mambo vipi?"
Salama vipi wewe?
"Salama tu,unaongea na  Queen."
Anhaaa za huko queen?
"Salama tu,ila Naomba kuongea nawewe maana Nina shida sana"(alisisitiza queen).
Nakusikiliza( huku nikiagiza chakula kwa mama ntilie maeneo ya mgahawa.
" Rafiki yangu anamatatizo...ana mimba ya miezi miwili,alie mpa haoneshi dalili za kumjali na kwao wazazi wake ni wakali sana sasa unanishauri nimwambie nini?"
   Naomba umwambie ajifungue tu maana watoto adimu kupatikana( nilimwambia queen)
"Haiwezekani kubeba hiyo mimba kwani bado nasoma na wazazi wamenigharamia sana hadi hapa Nilipo fika,hawata nielewa".
Haaa! Kumbe niwewe umepata ujauzito?(Nikaacha chakula mezani nikatoka nje).
" Ndio,David naomba nisamehe najua nimekuumiza ila naomba nisaidie".
Wewe mwanamke wa ajabu sana umepewa mimba huko unaniomba mimi msaada,kwani ushawahi kulala nami?au nafahamu mwili wako?au we unaufahamu mwili wangu?Huoni aibu tu,nilijitoa kwako kwa hali yangu japo sio nzuri ukanidharau afu unaomba msamaha. Fikiria ungekuwa wewe ndio mimi unafanyaje?
Queen: Najua nilikukosea naomba nisamehe!
David  :Nishakusamehe...Ila kwa sasa wewe beba huo ujauzito hadi siku ukijifungua,wajomba tupo wengi mtoto hatoweza kukaa na njaa na hata ivo baba yake ipo siku atakuja kumfuata mwanae.
Queen: Mbona unaongea kwa hasira sana?Najua ulinipenda lakini sikutambua upendo wako,naomba nisamehe najua umeumia sana juu yangu.
Isaac naye akawa anatoka nje baada ya kumaliza kula huku akiwa kabeba chakula changu kwenye "take away hotpot"...
Isaac: Vipi kuna tatizo?
Ndio kuna tatizo.(Nilijibu Wakati huo bado sikuwa nimekata simu)




NDOTO SEHEMU YA TATU.


        Nikakata simu aliyokuwa kapiga Queen.Isaac alihitaji maelezo ya tatizo nililo kuwa tayari nimemweleza kuwa nina tatizo.
   Niliweza msimulia mwanzo hadi mwisho yaliyo tokea lakini Isaac alishauri hivi" kama kumsikiliza,msikilize,na kama kumsaidia msaidie kama kuna kitu cha kumsaidi".
  Nilipomaliza maongezi nikaamua kula chakula na kuenda kulala ndani ya gari.Asubuhi ilipofika nikaenda kufungua tulubai ya gari.Nilipo maliza kufungua Isaac akaleta simu yangu iliyo kuwa ndani ya gari."simu yako inaita ila ni kama namba hujaihifadhi kwenye simu yako".nikapokea.."haloo..!
Queen:Habari ya asubuhi David.?
David. :Salama tu vipi wewe?
Queen:Safi tu..Jana niliweza mtafuta mpenzi wangu alienipa ujauzito,nilipo mweleza akaniambia,kwa sababu nasoma hakuna budi kuitoa ili niendelee na masomo.
David :Anhaaa! Mmeisha kubaliana si Ndio?
Queen: Ndio,amesema kesho niende kuonana na yeye anipeleke huko nikatoe....
David  :Okey.! Sasa sikiliza vyema,ukienda kesho kutoa.....usinitafute hadi wiki iishe siitaji matatizo..umenielewa?
Queen:Ndio nimekuelewa..
David. :Asante,Nina kazi muda huu,nikutakie siku njema,na kumbuka unachoenda kufanya usije poteza maisha yako.
Queen: Unanitishia David!
David. :Hapana ni ukweli kabisa nakueleza,siku njema.
  Nikakata simu na kuendelea na shughuli za kuhakikisha mzigo tulio upakia.Mzigo ulipo isha tukiwa tunajiandaa kuondoka..
"Mambo vipi suka?" (Mzee alisalimia tuliwa ndani ya gari)
Isaac: Poa vipi?
Mzee :Safi,samahani Nina mzigo wa maharage kama gunia mia na hamsini vipi mnaweza nipakilia hadi Tunduma?
Isaac: Ongea na kondakta..!
Mzee:Naomba nisaidie bwana..!(huku akinitazama)
"Naomba subiri kwanza niongee na mwenzangu juu ya swala hili" (nilimjibu mzee Yule,akashuka kwenye ngazi ya gari)
Isaac: Mi naona tupakie mzigo au we waonaje?
David : Poa,maana hata hela za kutumia sina.

Pia simulizi hizi zinapatikana kwanjia ya sauti kwa kubofya Hapa

PATA NYIMBO NZURI ZA INJILI, INTERVIEWS NA HABARI ZA MASTAA WA GOSPEL KUPITIA SACODE TV


 



KUWA WA KWANZA KUPATA MUSIKI WA INJILI KWA KUBOFYA HAPA

KUNAMBI SERVICES

HIFADHI ,MAGAZETI YALIYOTUMINA NA UZA HAPA